Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba wanavyoua, kujeruhi ng’ombe Serengeti

Simba wanavyoua, kujeruhi ng’ombe Serengeti

Fri, 6 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Siku moja baada ya simba kuuawa na askari wa wanyamapori baada ya kujeruhi mtu mmoja kijiji cha Robanda, wilayani Serengeti Mkoa wa Mara nchini Tanzania, ng'ombe watano wameuawa na simba na kujeruhi mmoja katika vijiji vitatu.

Vijiji hivyo ni vya Robanda, Nyichoka na Bukore wilayani humo.

Akizungumza leo Ijumaa Desemba 6, 2019, Ofisa mtendaji wa kijiji cha Robanda, Itabe Nkiri amesema hao waliouawa na kujeruhiwa ni mali ya Samwel Mahewa.

Amesema Novemba 3, 2019 simba hao waliua ng'ombe 21 mali ya Mahewa na jana Alhamisi wakajeruhi aliyekuwa mchungaji wake na usiku wakaingia na kuua ng'ombe watano.

Ofisa mtendaji wa kata ya Kyambahi, Mohammed Hamisi amesema katika kijiji cha Bokore wameua ng'ombe mmoja na kujeruhi mmoja Nyichoka ambako walivamia juzi.

Mmoja wa maofisa toka Grumeti Fund, David Mwakipesile amesema usiku huo walisaidia kuokoa mifugo kwenye mazizi manne na wameweka gari moja kwa ajili ya ulinzi.

Chanzo: mwananchi.co.tz