Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simanzi mazishi ya mwanaume aliyebanwa nyeti na mkewe kisha kuchomwa kisu

Kisuu?fit=612%2C408&ssl=1 Simanzi mazishi ya mwanaume aliyebanwa nyeti na mkewe kisha kuchomwa kisu

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vilio, simanzi na huzuni imetawala katika mazishi ya aliyekuwa Ofisa Kilimo Kata ya Neruma Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Julius Lubamba, anayedaiwa kufariki kwa kubanwa 'nyeti' zake na kuchomwa kitu chenye ncha kali mwilini mwake na mke wake, Elizabeth Steven (30).

Maziko ya mwili wa ofisa kilimo huyo yamefanyika jana Alhamisi Aprili 4, 2024, katika makaburi ya familia yaliyopo nyumbani kwao mtaa wa lsela Kata ya Usagara wilayani Misungwi mkoani Mwanza huku maelfu ya wananchi wakiungana na ndugu kuhitimisha safari ya Julius duniani.

Nicolaus Mzee ambaye ni msemaji wa familia ya marehemu, akizungumza baada ya shughuli ya kuaga mwili huo anatoa msimamo wa familia hiyo kuhusiana na kifo cha mpendwa wao.

Kifo cha Julius, siyo tu kimeacha majonzi kwa familia, pia kimewagusa marafiki na wanafunzi waliosoma naye akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi mkoani Mwanza, Kashinje Masanja ambaye anaitupia lawama Sera ya usawa wa kijinsia akidai imechangia tukio hilo kutokea.

Hata hivyo, Mchungaji wa Kanisa la PAG Tanzania, Amos Festo amewataka ndugu wa marehemu kumuombea wa kile alichodai mtuhumiwa amefanikiwa kuondoa uhai wake na siyo roho yake huku akiwataka waombolezaji kumrudia Mungu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live