Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simanzi mazishi ya binti aliyesombwa na maji Morogoro

Mazishi Binti Moro Simanzi mazishi ya binti aliyesombwa na maji Morogoro

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamia ya wananchi wa Mkoa wa Morogoro leo Jioni wamejitokeza kwa wingi kumzika mwanafunzi wa darasa la tatu, Sabrina Abdallah aliyefariki dunia juzi jioni baada ya kusombwa na maji ya Mto Morogoro..

Mwenyekiti wa Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro, Hashim Bito ambaye alithibisha kuwa mwanafunzi huyo alisombwa na maji.



Sabrina alikuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mwere ‘B’, alifariki dunia juzi Dersemba 6, baada ya kuteleza kwenye kina kirefu cha maji ya Mto Morogoro majira ya saa 9 alasiri muda mfupi baada ya kutoka shuleni.

Sabrina amezikwa jana saa 9 Alasiri katika Makaburi ya Kolla huku Umati Mkubwa wawanchini kutoka maeneo mbalimbali ulijitokeza kushiriki mazishi hayo.

Simbanzi na vilio vilitawala kwa ndugu jamaa na marafiki, hasa wanafunzi wenzake wa darasa la tatu aliyokuwa akisoma nao ambao walifika kwa ajili ya kushiriki mazishi ya mpendwa wao huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live