Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simanzi bibi anayeishi kwenye nyumba ya mianzi

Kikongwe Tulia.png Simanzi bibi anayeishi kwenye nyumba ya mianzi

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: Wasafi tv

Eneva Kaseghe ni bibi wa miaka 67 mwenye uhitaji anayeishi katika Kijiji cha Kibisi kata ya Kyimo Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Bibi huyo aliyepata ulemavu wa viungo baada ya mumewe na watoto wake kufariki Dunia , anaishi katika mazingira hatarishi akiwa katika nyumba iliyo simamishwa kwa miamzi na kuezekwa turubai, ambayo kwasasa vimeoza na kufanya bibi Eneva kua katika mazingira hatarishi zaidi hasa katika kipindi hiki Cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Hali hiyo imewavuta taasisi ya Tulia Trust, iliyo chini ya Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson, ambao wamefika katika Kijiji Cha Kibisi anapoishi bibi Eneva na kuwataka mtendaji wa kata ya Kyimo kwa kushirikiana na mwenyekiti wa Kijiji Cha Kibisi, kuainisha mahitaji yake ya muhimu Ili aweze kisaidiwa kwa haraka kutokana na hatari iliyopo katika makazi yake.

Kwa upande wao baadhi ya majirabi wa bibi Eneva Kaseghe, nao wakapata wasaa wa kueleza hali halisi ya maisha ya jirani yao ambaye alikua akifanya biashara zake vyema kabla ya mumewe nawatoto wake kufariki, na baada ya hapo ndioo alianza kuugua mara kwa mara hali iliyo mpelekea ulemavu wa miguu alionao hivi Sasa.

Chanzo: Wasafi tv