Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simanzi! Watoto wawili waliouawa kwa kukatwa mapanga wazikwa

Vilio Picm Simanzi! Watoto wawili waliouawa kwa kukatwa mapanga wazikwa

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vilio na simanzi vimetawala leo Ijumaa Novemba 25, 2022 wakati miili ya watoto Neema Chembe (7) na Leonard Chembe (1) ilipowasili nyumbani kwao eneo la Ilolo kata ya Sisimba jijini Mbeya.

Watoto hao ambao walifiriki dunia baada mama yao mzazi Shari Mwambamba (27) kuwakata kwa mapanga katika maeneo ya kichwani na mikononi wakiwa ndani ya nyumba.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga tukio hilo lilitokea Jumatano, Novemba 23, 2022 eneo la Ilolo, Kata ya Sinde, Tarafa ya Sisimba.

Leo Ijumaa Novemba 25, 2022 mamia ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wamefika msibani kwenye mazishi ya watoto hao, huku baadhi wakiwa kwenye makundi wakijadili tukio hilo.

Juma Mwashilindi mkazi wa Ilolo amesema kitendo kilichofanywa kinaleta maumivu makali na hakivumiliki licha ya kuwepo kwa sababu kuwa amekutwa na tatizo la afya ya akili.

“Tukio hilo limeacha simanzi kubwa kwani amekatisha ndoto za watoto hao na hata kama aligundulika kuweweseka mume wake alipaswa kumkamata na kumpeleka hosptali kabla ya kutokea madhara makubwa”amesema.

Naye, Sophia Aron amesema kuwa tukio hilo limewaliza kwani hawakuwai kuona mama wa watoto hao akiwa na tofauti zozote za kiafya na alikuwa kipenzi kikubwa cha watoto wake.

Wakati huo huo baba wa watoto hao, Evalist Chembe amesema kuwa tangu waanze maisha na mkewe miaka kumi iliyopita haijawai kutokea kuwa na roho ya kikatili ya kufikia hatua ya kufanya mauaji.

“Nashindwa hata niseme nini ingawa mke wangu kabla ya Novemba 23, 2022 kufanya tukio hilo alikuwa akiweweseka sana usiku, hali hiyo ilimkuta tangu afariki mdogo wake kwa kujinyonga wilayani Mbarali ”amesema.

Aliongeza kuwa “Tangu tumzike mdogo wake hali yake haikuwa sawa na nililazimika kumuita mdogo wake ambaye naye alijeruhiwa kwa ajili ya kumpeleka kwenye matibabu”amesema.

Awali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo lilitokea  Novemba 23,2022 majira ya saa 3.00 ambapo  watoto wawili waliuwawa kwa kukatwa kwa panga na wengine wawili   akiwepo mtoto Emmanuel Chembe (3) na Nuru Yonem kujeruhiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live