Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simanzi! Umeme wa jua wateketeza nyumba

Umeme Jua Mds.jpeg Umeme wa jua wateketeza nyumba

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simanzi na vilio vimetawala kwenye familia ya Lenard Ramadhani na Happyness Richard, wakazi wa mtaa wa Tulieni, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi baada ya nyumba yao kuteketea kwa moto huku chanzo kikitajwa kuwa ni umeme wa jua na kuokoa pikipiki na sofa seti moja pekee.

Kamanda wa jeshi la zima moto mkoa wa Katavi, Regina Kaombwe, amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo wamiliki wa nyumba hiyo kutokana na nyakati wanayopitia wamegoma kuzungumza chochote huku wakimueleza mwandishi kuwa tatizo limekwisha tokea hata wakizungumza haisaidii chochote.

Kamanda Regna amesikitishwa na kitendo cha wananchi wa mtaa huo kushindwa kutoa taarifa mapema pindi moto ulipozuka na kuwaomba wananchi wajenge tabia ya kutoa taarifa mapema ili waweze kuokoa mali na sio kuzima moto pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live