Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simamieni haki za wanaohama Ngorongoro

Kairuki Pic Simamieni haki za wanaohama Ngorongoro

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki amemwapisha Kamishna mpya wa Hifadhi ya Ngorongoro Richard Kiiza na kumtaka kusimamia zoezi la kuhama kwa hiari kwa watu wa jamii ya kimasai katika hifadhi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kumvisha cheo na kumwapisha Kamishna huyo, Waziri Kairuki amesema uteuzi huo ni sehemu ya kuimarisha timu ya utekelezaji wa majukumu ya Uhifadhi na utalii.

Amesema katika awamu ya pili ya utekelezaji wa zoezi hilo, Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa zoezi la kuhamisha wananchi kwa hiari ikiwemo ujenzi wa Nyumba 5,000 katika Kijiji cha Msomera Wilayani Handeni, Saunyi Wilaya ya Kilindi na Kitwai Wilaya ya Simanjiro ili kuhakikisha Wananchi walio tayari kuhama wanapata makazi bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live