Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Silaa asitisha ujenzi kituo cha mafuta Moshi

Sd Silaaa Silaa asitisha ujenzi kituo cha mafuta Moshi

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, Jerry Silaa ameitaka Manispaa ya Moshi kusitisha kibali cha ujenzi wa kituo kidogo cha mafuta kwenye kiwanja kilichopo kata ya Mawenzi Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, ambacho kimeorodheshwa katika taarifa ya maeneo yaliyotajwa kuwa maeneo ya wazi kwa sababu ya kutokuzingatia mpango Mji na amewataka Watalaamu wa Ardhi waliotoa kibali cha ujenzi wa kituo hicho kusimamisha ujenzi huo haraka iwezekanavyo.

“Nimeona ipo tabia hiyo inayokithiri ya kubadilisha matumizi ya maeneo kuwa ya vituo vya mafuta pasipo kuzingatia matumizi mengine yaliyopo kwa mfano pale Dar es salaam kuna kituo kipo karibu kabisa na Shuls na nyinyi ndo mmegawa kiwanja hiko na kubadilisha matumizi ya eneo hilo ambalo lilikuwa linatumika kama eneo la mapumziko na kuwa kituo cha mafuta”

Waziri Silaa ameyasema hayo jana October 5 2023, wakati wa ziara yake Mkoani Kilimanjaro ambapo alikuwa akipokea taarifa ya maeneo yaliyotajwa kuwa maeneo ya wazi.

“Nyie wenyewe ni Mashahidi kuwa hata Serikali yenyewe inapata changamoto ya upatikanaji wa maeneo ya huduma yakiwemo ya ujenzi wa vituo vya afya na Shule na kulazimika kuingia gharama kubwa ya kupata ardhi kwa ajili ya huduma hizo lakini hata yaliyopo mnashindwa kuyalinda na mnayapangia matumizi mengine, leo kabla sijatoka Moshi nione hiyo amri ya kusimamisha”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live