Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Sikufa ajalini, nipo hai’

Simulizipic Data ‘Sikufa ajalini, nipo hai’

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mmoja wa madereva wa gari la magazeti lililopata ajali juzi katika eneo la Lungumba, Mahenge Mkoani Iringa, Abdul Ally Lyuu amesema yupo hai isipokuwa alisahau leseni yake kwenye gari hilo ndiyo maana alitajwa katika orodha ya waliopoteza maisha.

Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, ACP Alan Bukumbi amesema kwa kawaida miili watu inapokuwa imeharibika vibaya kiasi cha sura zao kutoonekana, vitambulisho ndivyo huwa vinatumika kujua majina ya waliokuwepo.

Lyuu sio kati ya watu 10 walio fariki kwenye ajali hiyo ambayo pia ilijeruhi watu wawili ikihusisha gari aina ya hiece mali ya Soma General Traders, isipokuwa aliacha leseni yake.

Akizungumza na Mwananchi, Lyuu alisema naye ni miongoni mwa madereva wa gari hilo lakini siku ya ajali hakusafiri isipokuwa alicha leseni yake huku madereva wengine.

"Nilisahau leseni yangu kwenye gari na wenzangu walipoondoka hawakujua kama ipo hivyo mimi nipo hai. Nimesoma kwenye mtandao nikaona jina langu limetajwa kati ya walio fariki," alisema Lyuu.

Ajali hiyo ilihusisha gari namba T249 DWT aina ya Toyota Hiace iliyokuwa inasafirisha magazeti kutoka Dar es Salaam kwenda mbeya.

Advertisement Akizungumzia hali ya majeruhi wawili, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Dkt Idd Omary amesema Monica Phill aliamua kwenda kuendelea na matibabu nchini kwao Malawi.

"Hapa tunae dereva ambaye tunatarajia kumpa rufaa ili akapate matibabu kwenye hospitali kubwa zaidi," amesema Dkt Omary.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz