Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku ya kimondo Songwe

62061 Kimondo+pic

Tue, 11 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbozi. Mkoa wa Songwe unatarajia kuazimisha siku ya Kimondo Duniani Juni 28-30, kwa kufanya maonyesho mbalimbali ya biashara ikiwemo mashindano ya baiskeli, mbio za nusu marathoni ikiwa ni njia ya kutangaza na kukuza utalii.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe,  Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela amewaambia waandishi wa habari leo Jumatatu kuwa maadhimisho hayo ambayo yalianza mwaka jana yanaendelezwa ili kukitangaza kimondo cha Mbozi na kuvutia watalii ili kupitia siku hiyo fursa za utalii zilizopo mkoani hapa ziweze kutangazwa.

Amesema maadhimisho hayo yatahudhuriwa pia na wageni mbalimbali kutoka mikoa mingine nchini na wengine kutoka nje ya nchi, na pia itatolewa elimu ya anga kuwafanya waelewe kuhusu vimondo vinavyotokea.

“Kupitia maadhimisho hayo, yatafanyika mashindano ya baiskeli kwa wanaume na wanawake, mbio za nusu marathoni, mashindano ya mapishi ya vyakula vya asili, ngoma za asili na mashindano mengine mengi,  pia zawadi mbalimbali zitatolewa"amesema  Mwangela.

Chanzo: mwananchi.co.tz