Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amewataka wafanyabiashara wadogo Maarufu Machinga kutumia Siku Mbili zilizobaki kabla ya Octoba 18 kuanza kuondoka kwenye maeneo yasiyofaa na kuelekea katika Maeneo Waliyopangwa rasmi ili waendelee na Biashara zao.
Ametoa Wito huo wakati alipokutana na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na Maafisa biashara kutathmini Mpango huo wa Serikali ambapo kazi ya Kubaini Maeneo rafiki ya Kibiashara yakiwemo Masoko Imekamilika.
"Kuna Wilaya ambazo zimepata neema tayari fedha zimetengwa kwaajili ya kuboresha miundombinu rafiki kwa machinga, naomba tutimize lengo la Waziri wa TAMISEMI, hivyo niwaombe machinga watii agizo hili kwani nia ya Serikali ni njema" RC Makalla