Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Siku 8 kufa, kupona NHC

Siku 8 kufa, kupona NHC

Mon, 23 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki siku nane kukamilisha mwaka, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetakiwa ifikapo Januari kuhakikisha limewachukulia hatua wapangaji wote wanaodaiwa jumla ya Sh8.23 bilioni malimbikizo ya pango.

Agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula alipokutana na menejimenti ya shirika hilo.

Mabula alisema katika kuifanya NHC inaimarika kimapato lazima madeni ya wapangaji wake yakusanywe kwa kuanzisha operesheni maalumu inatakayowezesha kutambuliwa wadaiwa wote na walipe kwa wakati.

“Ukiacha zile taasisi za Serikali, wote wanaodaiwa ikifika Januari 2020 wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na zile taasisi za umma mkamuone katibu mkuu Hazina ili zikatwe fedha moja kwa moja,” alisema Mabula.

Awali, mkurugenzi wa umiliki na uendelezaji NHC, Greyson Godfrey alisema licha ya shirika kuimarika katika makusanyo, liko kwenye mikakati maalumu wa kukusanya madeni kwa wadaiwa kwa kuingia makubaliano maalumu namna watakavyolipa.

Naye mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Dk Maulid Banyani alisema wamekuwa na mikakati mbalimbali kuhakikisha wanaimarika kimapato ikiwamo kutoa motisha kwa watumishi wanaofanya vizuri mikoa itakayofikia lengo la makusanyo na kutokana na malimbikizo ya m

Pia Soma

Advertisement
Dk Banyani alisema kwa sasa NHC imeanza uhakiki kwa wapangaji wake kubaini waliopangisha wengine na eneo la Ubungo limetumika kama majaribio tayari wapangaji sita wameondolewa.

Katika hatua nyingine, Mabula aliagiza kupatiwa orodha ya nyumba zote za NHC zilizouzwa, zisizouzwa, zilizopangishwa na zisizopangishwa na viwanja visivyoendelezwa.
Chanzo: mwananchi.co.tz