Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sikonge yajipanga kwa bajeti ya bilioni 28.3/-

07872d9f7b1545a2e038c878f40e00a7 Sikonge yajipanga kwa bajeti ya bilioni 28.3/-

Sun, 4 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

HALMASHAURI ya Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora inatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha Sh bilioni 28.3 katika bajeti yake ya mwaka wa fedha wa 2021/22 kwenye shughuli za maendeleo.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (FDC) wilayani humo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Rashid Magope alisema kati ya fedha hizo Sh bilioni 20.1 ni matumizi ya kawaida na Sh bilioni 8.2 ni za miradi ya maendeleo.

Alibainisha kuwa katika mwaka ujao wa fedha, halmashauri hiyo inakusudia kukusanya kiasi cha Sh bilioni 3.2 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani.

Alisema bajeti ya mwaka ujao imepanda kwa asilimia 11.7 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha uliopita 2020/21 ambayo ilikuwa Sh bilioni 25.3.

Magope alifafanua vipaumbe vya bajeti ya mwaka ujao kuwa ni kukuza uchumi na maendeleo ya viwanda , kuimarisha miundombinu ya elimu, afya, kujenga skimu za kilimo cha umwagiliaji cha zao la mpunga katika bonde la Kalupale lenye ukubwa wa hekta 2,008.

Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni uanzishaji wa mashamba makubwa ya kilimo cha mazao ya kudumu kama vile miembe na korosha, kukamilisha jengo la Utawala la Halmashauri, ujenzi wa viwanda vidogo na kukatua kero za wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo Peres Magiri alishauri halmashauri kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ili kufanikisha vipaumbele vya bejeti hiyo ikiwemo kuimarisha kilimo chenye tija ambacho kitachochea uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula ili kuinua uchumi wa wananchi.

Aliongeza kuwa serikali imekuwa ikisisitiza kila halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato ili iweze kuongeza mapato yake ambayo yataiwezesha kutekeleza miradi ya maendeleo kwa asilimia 100 ikiwemo kutenga asilimia 10 kwa ajili ya hayo kuwezesha vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kiuchumi.

Aidha aliwataka madiwani kushirikiana na wataalamu, watendaji na jamii kwa ujumla katika kuhamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuinua kiwango cha ufaulu katika mitihani yao.

Alisema hatua hii inakwenda sambamba na mapambano dhidi ya utoro sugu miongoni mwa wanafunzi ikiwemo kuwachukulia hatua wahusika kwa mujibu wa Sheria.

Magiri alimuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi, wilayani humo kuendesha oparesheni ya kukamata watoto wote watakaokutwa wakicheza kamari au mchezo wa pulu (pool) wakati wa saa za masomo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz