Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule zote 190 wilayani Serengeti zapewa majiko ya gesi

Mitungi Nya Gesi Bei.png Shule zote 190 wilayani Serengeti zapewa majiko ya gesi

Wed, 17 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shule zote 190 za umma za msingi na sekondari za Wilaya ya Serengeti zimepata msaada wa majiko ya gesi kwa ajili ya matumizi ya walimu wakati wa kujiandalia chakula wawapo kazini.

Majiko hayo yenye thamani ya zaidi ya Sh9.5 milioni yametolewa na mdau wa maendeleo Wilaya ya Serengeti, Rhimo Nyansaho kuitikia ombi la Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) wilayani humo.

Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) Kitengo cha Wanawake Wilaya ya Serengeti, Grace Mutaengerwa amesema msaada huo utanufaisha jumla ya walimu 1, 753 katika shule za msingi na sekondari wilayani humo. Also Read

Wafanyabishara: Mfumo wa kodi ufumuliwe tupumue Kitaifa 26 min ago Wafanyabishara: Mfumo wa kodi ufumuliwe tupumue Kitaifa 26 min ago

‘’Walimu wetu wanatumia muda mwingi kujiandali hata chai wawapo shuleni kutokana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa; msaada huu utamaliza tatizo hilo, hivyo walimu kutumia muda mwingi darasani,’’ amesema Grace

Akikabidhi majiko hayo kwa baadhi ya wakuu wa shule na walimu wakuu leo Mei 17, 2023, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Dk Vicent Mashinji amempongeza Rhimo kwa msaada huo huku akiwaomba wadau wengine kujitolea kusaidia upatikanaji wa majiko ya gesi kwa makundi yenye mahitaji maalum na taasisi zinazohudumia watu wengi kwa mahitaji ya chakula.

Dk Mashinji ametaja magereza na taasisi za elimu zikiwemo shule za bweni na vyuo vya kati kuwa miongoni mwa taasisi zinazohudumia watu wengi zinazohitaji kuanza kutumia nishati ya gesi badala ya kuni na mkaa.

‘’Matumizi ya nishati ya gesi itapunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na kuchoma mkaa kwa ajili ya gesi; na hivyo kuokoa mazingira,’’ amesema Dk Mashinji

Akitoa shukrani kwa niaba ya walimu, Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Serengeti, Lusawi Mayala amewaomba wadau wengine wa elimu ndani na nje ya wilaya hiyo kujitokeza kusaidia maendeleo ya sekta ya elimu kwa kuboresha miundombinu na mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Mwenyekiti huyo amewaomba walimu wanaonufaika na misaada ya wadau kuitumia kwa malengo yanayokusudiwa ili ziwe endelevu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live