Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule za Kinondoni ‘zinavyokimbiza’ ufaulu Dar

42591 Pic+kino Shule za Kinondoni ‘zinavyokimbiza’ ufaulu Dar

Tue, 19 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Baadhi ya wanafunzi nchini Uingereza wameingia mitaani kwa mabango kujiunga na maandamano ya kupinga ongezeko la joto duniani na kuunga mkono juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchini.

Viongozi walioongoza harakati hizo wakiwamo wanasiasa walipongeza hatua ya kundi la wanafunzi wakiwamo wa vyuo mbalimbali kwa kusitisha masomo yao kwa muda na kujiunga na harakati za kupinga ongezeko la joto duniani.

Waziri wa Nishati wa nchi hiyo Claire Perry alisema anajivunia kuona vijana jasiri na imara wanaotambua wajibu wao na kuchukua hatua za kuunga mkono juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchini.

Mbali na pongezi za waziri huyo kwa wanafunzi waliojitokeza mitaani pia baadhi ya viongozi wakiwamo mawaziri wa zamani walitumia akaunti zao kwenye mitandao ya kijamii kuwapongeza wanafunzi hao kuwa ni somo bora la uraia kwa mwaka huu.

Akizungumza na waandamanaji hao wakiwamo wanafunzi hao,Mbunge wa Newbury Richard Benyon, alisema anajivunia mafanikio ya nchi hiyo katika kupunguza uzalishaji wa gesi na ulinzi wa mazingira ya bahari na kukomesha uzalishaji wa umeme kwa makaa ya mawe.

Hata hivyo, msemaji wa Elimu alisema ni vizuri watu kushiriki katika masuala wanayodhani yana athari kwao na kuonyesha kuwa wanajali na kuonya jambo lililofanywa na wanafunzi hao haliwezi kuleta mabadiliko yoyote kwenye mazingira zaidi ya kuwaongezea walimu wao kazi ya ziada darasani.

The Guardian



Chanzo: mwananchi.co.tz