Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule ya Msingi Narwadi yajenga choo cha kudumu baada ya miaka 22

Shule ya Msingi Narwadi yajenga choo cha kudumu baada ya miaka 22

Sat, 21 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lindi. Zaidi ya wanafunzi 140 wa shule ya Msingi Narwadi halmashauri ya Mtama mkoani Lindi sasa hawatajisaidia kwenye vichaka baada ya kukamilika kwa ujenzi wa vyoo bora vya kisasa  vya kudumu vyenye mfumo wa maji.

Hiyo ni mara ya kwanza tangu  kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 1997.

Ujenzi huo wa vyoo ulitekelezwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Heart to Heart kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini kupitia Shirika la Maendeleo la Korea Cooperation Agency (Koica).

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Zamda Issa amesema tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 1997 haijawahi kuwa na vyoo bora na kusababisha wanafunzi kujisaidia kwenye vichaka kutokana na choo kilichopo kilichoezekwa kwa udongo kutishia usalama.

Mratibu wa mradi huo, Abraham Msofe amesema watatumia  zaidi ya Sh2.8 bilioni kwa ajili kuchimba vyoo katika baadhi ya shule na kuchimba visima vya maji katika baadhi ya vituo vya afya na shule wilayani Lindi.

“Idara ya elimu na afya wamekuwa wanufaika wa mradi amejikita katika ujenzi wa vyoo na uchimbaji wa visima virefu ili kupata maji safi na salama lakini pia kuwezesha usafi katika shule na vituo vya afya. Pia kuwezesha watu wanaotoka chooni kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na kuepuka magonjwa, “amesema Msofe

Kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya Mtama, Dk Dismas Stephen amesema  licha ya shule hiyo kupata vyoo bora bado hali ya vyoo vya wananchi sio nzuri na kuwataka kujenga vyoo bora kabla ya Februari 2020.

 

Mkurugenzi wa  halmashauri hiyo, Samwel Waryuba  amesema, “tujitahidi tufanye kazi kwa sababu bila kazi choo kitakushinda kujenga. Tangu  nchi ipate uhuru mpaka sasa ni miaka 58, umri wa mtu mzima lakini unataka kujisaidia unakwenda kwenye kichaka, hii ni aibu.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz