Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule ya Msingi Msasani yafurika maji, wanafunzi 487 hawajafika shuleni

56655 Shulemvuapic

Fri, 10 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam kuanzia leo alfajiri Ijumaa Mei 10, 2019 na kusababisha baadhi ya madarasa ya  shule ya msingi Msasani kujaa maji na kuathiri shughuli mbalimbali shuleni hapo.

Akizungumza na Mwananchi leo mwalimu mkuu wa shule hiyo,  Edward Molel amesema kutokana na hali hiyo mahudhurio ya wanafunzi yamepungua na hali ya ufundishaji imekuwa ngumu.

Amesema kwa kawaida shule hiyo mvua zikinyesha madarasa matatu ndiyo hujaa maji, lakini kwa mvua zinazoendelea kunyesha kwa siku ya tatu mfululizo, madarasa matano yamejaa maji pamoja na yake.

"Shule ina wanafunzi 647, lakini kutokana na mvua hizi wamekuja 160 huku wa darasa la kwanza na la pili hawajafika kabisa" amesema mwalimu Molel.

Haya hivyo Molel amesema kuwa wiki mbili zilizopita kiasi cha Sh 5.2 milioni kimeingizwa kwenye akaunti  kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.

"Fedha hizo ni kwa ajili ya kuchimba mtaro nyuma ya shule ambako ndiyo eneo korofi, mtaro huo utakuwa unapokea maji kwenda kwenye mifereji mikubwa ambayo inayapeleka baharini" amesema Molel.

Habari zinazohusiana na hii

Molel ameiomba Serikali na wadau wa elimu wa eneo hilo kumjengea ofisi pamoja na ofisi ya walimu kwa sababu zilizopo zinajaa maji na zimeshaharibiwa na hali hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz