Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule ya Msingi Keza hatarini kufungwa kwa kukosa vyoo

Chooooooo Shule ya Msingi Keza hatarini kufungwa kwa kukosa vyoo

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shule ya Singi Keza Wilayani Ngara, hatihati kufungwa kwa ukosefu wa vyoo unaopelekea mazingira ya shule kuwa magumu kufundisha na kujifunzia.

Baada ya kipande cha video kusambaa mitandaoni ikiwaonesha Wanafunzi na Walimu wakilalamikia hali ya shule hiyo, Mbunge wa Jimbo la Ngara, Ndaisaba George Ruhoro amesema;

“Nilifika shuleni nikatoa Tsh. Milioni 3 ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ambayo ilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya dharura na Ths. Milioni 15 ya vyanzo vya ndani vya Halmashauri.”

Ameongeza kuwa tayari ujenzi unaendelea na kuongeza “Shule ya Keza ilijengwa Mwaka 1945 wakati wa Vita vya Dunia, miundombinu inatakiwa kufanyiwa maboresho.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live