Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule tatu za msingi zageuzwa sekondari Dar

91276 Shule+pic Shule tatu za msingi zageuzwa sekondari Dar

Fri, 10 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shule tatu za msingi zimebadilishwa na kuwa sekondari ili kukabiliana na wanafunzi waliofaulu darasa la saba na kukosa madarasa.

Hayo yalisemwa jana na ofisa elimu mkoa wa Dar es Salaam, Hamis Lissu katika mahojiano maalumu na Mwananchi iliyotaka kujua kama wanafunzi wote waliofaulu wamepata shule.

Lissu alisema wamefamnikiwa zaidi ya wanafunzi 69,000 waliofaulu wote wamepata shule, huku akizitaja shule zilizobadilishwa ni Kijitonyama, Magomeni na Muungano.

“Shule hizo ambazo kila moja ina uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 200, zitapunguza tatizo hilo, zaidi ya wanafunzi 69,000 waliofaulu mitihani yao wamepata nafasi kuanza kidato cha kwanza Januari 6,” alisema Lissu.

Kuhusu iwapo haitaleta athari kwa wanafunzi wa shule za msingi, Lissu alisema hakuna athari zozote ikizingatiwa shule wanazozibadili zipo mbili sehemu moja.

Kama vile haitoshi, alisema wanaangalia idadi ya wanafunzi waliopo shule husika, kutokana na wazazi wengi kuhamia nje ya mji baadhi ya shule zimekuwa na wanafunzi wachache hivyo kuwahamishiwa shule jirani.

Licha ya mafanikio hayo, Lissu alisema changamoto zipo katika madawati na kuomba wadau kujitokeza kuchangia kwa kuwa shule zinaendelea kujengwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz