Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule sita Kanda ya Ziwa kidedea matokeo darasa la saba

23577 Matokeo+pic TanzaniaWeb

Wed, 24 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetaja shule 10 bora kitaifa zilizofanya vizuri katika matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi, huku mikoa iliyopo Kanda ya Ziwa ikitoa  shule sita katika orodha hiyo.

Shule hizo ni Nyamuge (Mwanza), Twibhoki (Mara), Kwema Modern na Rocken Hill (Shinyanga),  Jkibira, St Achileus Kiwanuka, St Severine na Rweikiza (zote Kagera).

Shule iliyoshika nafasi ya kwanza katika shule 10 bora ni  Raskazone ya Tanga huku St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam ikishika nafasi ya sita.

Pia,  wanafunzi sita kati ya 10 waliofanya vyema kitaifa katika mtihani huo pia wanatokea shule za kanda ya ziwa.

Akitangaza matokeo hayo leo Oktoba 23, 2018  Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema ufaulu umepanda kwa asilimia 4.96.

Wanafunzi bora

Dk Msonde amewtaja watahiniwa 10 bora kitaifa na shule zao kwenye mabano ni Ndemezo Lubonankebe (Kadama-Geita), Innocent Seleli (Carmel-Morogoro), Given Malyango (Tumaini Junior –Arusha), Diomedes Mbogo (St Achileus Kiwanuka-Kagera), Sweetbert John (Mingas-Shinyanga).

Najma Manji (Nyamuge-Mwanza), Beatrice Jeremiah (Mapinduzi B-Mara), Mohamed Abdirahman Mohamed na Luqman Ally (Raskazone-Tanga) na Francisco Maiga (Kadama-Geita).

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz