Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule shikizi yakosa madawati

Dadaa Wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye matofali

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: eatv.tv

Shule shikizi ya Lerug, iliyopo Kijiji cha Lerug wilayani Kiteto mkoani Manyara, iliyojengwa kupunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali wa KM 20 hadi 25 kufika shule mama ya Kijungu, kwa sasa inakabiliwa na uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa hali inayochangia kushuka kwa kiwango cha cha elimu kwa watoto kutokana na mazingira kuwa duni.

Shule hiyo ilianzishwa mwaka 2012 na haijasajiliwa hivyo inatambulika kama shule shikizi yenye lengo la kupunguza adha ya wanafunzi hao kutembea umbali mrefu km 25 kwenda shule mama ya Kijungu wilayani Kiteto.

Mwalimu wa shule hiyo Moi Mainge Lemalai, amesema kuwa shule hiyo bado haijasajiliwa na kwamba licha ya upungufu wa madarasa wananchi walianza kujenga baadhi ya madarasa kwa nguvu zao lakini bado hakuna unafuu unaostahili huku pia shule hiyo ikikabiliwa na uhaba wa walimu.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lerug Kitoni Sebore, amekiri kuwa hali ya kielimu ni tete kijijini na kuomba serikali kuwanusuru hao wanafunzi makalio yao yataisha kwani tofali za saruji zinaumiza.

Chanzo: eatv.tv