Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule nane za msingi Dar kuwa za sekondari

Thu, 17 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katika kuhakikisha wanafunzi waliofaulu kwenda sekondari na kukosa nafasi hawaachwi nyuma kimasomo na wenzao, Mkoa wa Dar es Salaam umewatafutia shule nane za msingi kwa muda ili waendelee.

Shule hizo pia ziko katika hatua ya mwisho kubadilishwa kuwa za sekondari.

Akizungumza na Mwananchi jana, ofisa Elimu (Taaluma) Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Nsuza alizitaja kuwa ni Mashujaa iliyopo Ubungo; Muungano, Ndalala, Serengeti, Kurasini na Minazini za Temeke.

Nyingine ni Mivinjeni na Buguruni Moto zilizopo katika Wilaya ya Ilala.

Alisema wanafunzi wa msingi waliokuwa wakisoma katika shule hizo tayari wamehamishiwa kwenye shule nyingine za karibu.

Alisema baada ya kufanywa kwa utafiti, shule hizo zimebainika kuwa na wanafunzi wachache na madarasa yake mengine yalikuwa hayatumiki kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wazazi kuhamia nje ya Dar es Salaam.

Akitoa mfano, aliitaja Shule ya Msingi Mashujaa iliyokuwa na vyumba 22 vya madarasa ambavyo vilikuwa havitumiki kwa takribani mwaka mzima.

Alisema tayari hatua za kuzisajili shule hizo kuwa za sekondari zinaendelea na huenda kuanzia Januari mwakani zikaanza kupokea wanafunzi.



Chanzo: mwananchi.co.tz