Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule iliyoongoza matokeo kidato cha nne 2019 yataja siri ya mafanikio

91411 Pic+shule Shule iliyoongoza matokeo kidato cha nne 2019 yataja siri ya mafanikio

Fri, 10 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) jana Alhamisi Januari 9, 2020 ilitangaza matokeo ya kidato cha nne 2019 huku Shule ya Sekondari Kemebos mkoani Kagera ikiibuka mshindi wa kwanza.

Matokeo ya mwaka 2018, shule hiyo ilikuwa ya pili huku St Francis Girls ya Mbeya ikishika nafasi ya kwanza lakini mwkaa 2019 St Francis imekuwa ya pili.

Katika matokeo hayo, Kemebos ilikuwa na watahiniwa 70, wasichana 26 na wavulana 44. Matokeo yanaonyesha wanafunzi wote wamepata daraja la kwanza yenye alama kati ya 7 hadi 10.

Meneja wa shule Kemobos, Eurogius Katiti amezungumza na Mwananchi shuleni hapo ambapo amesema amebainisha mikakati kadhaa iliyoifanya kuibuka kidedea.

Katiti ameitaja mikakati hiyo ni ushirikiano wa walimu, wanafunzi na viongozi wa shule kuwa timu moja na kumaliza silabasi ndani ya muda.

Amesema katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne 2019 yaliyotangazwa  jana, shule ya Kemebos imekuwa ya kwanza kitaifa na katika mtihani wa kidato cha pili imekuwa ya pili kitaifa na mtihani wa darasa la nne ya kwanza kitaifa.

"Katika matokeo ya kidato cha nne mwaka jana shule ilikuwa ya tatu kitaifa na leo tumepanda nafasi hivyo tunakibarua cha kuendelea kutetea nafasi hii ili shule yetu iendelee kuongoza kitaifa," amesema meneja wa shule hiyo Katiti.

Amewaomba walimu, wanafunzi na wazazi kuendeleza ushirikiano ili kuendelea kupata matokeo mazuri shuleni hapo na kuwa wazazi waendelee kuleta watoto wao Kemebos na Kaizirege ili wapate elimu bora.

Chanzo: mwananchi.co.tz