Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shule haina walimu, wananchi wachangisha fedha kuajiri walimu

Mwalimu Darasani 0?fit=700%2C444&ssl=1 Shule haina walimu, wananchi wachangisha fedha kuajiri walimu

Sat, 8 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mji Mpya iliyopo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameiomba Serikali kuwapatia walimu wa masomo ya Sayansi pamoja na kuweka vifaa katika maabara ya Kemia ili kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia ili kufikia malengo yao ya ufaulu.

Shule hiyo yenye wanafunzi 825 changamoto kubwa imetajwa kuwa kwa walimu wa Fizikia na Hisabati hali ambayo husababisha wakati mwigine wazazi kuchangia kiasi kdogo cha fedha ili kuajiri walimu wa muda wa kufundisha masomo hayo

Wakizungumza wakati wa kupokea meza na viti 100 kutoka kwa Mbunge wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo, wanafunzi hao wamesema kukosekana kwa walimu wa Sayansi kumewafanya kusoma katika mazingira magumu.

Akitoa taarifa Mkuu wa Shule hiyo, Charles Mkenda amesema wanakabiliwa na changamoto mbalibali na kwamba ukosefu wa walimu wa Sayansi umekuwa kikwazo kikubwa kwa wanafunzi wanaosoma masomo hayo na kwamba kuna wakati hulazimika kuchangisha wazazi ili kuajiri walimu wa muda

Alisema changamoto nyingine ni upungufu wa viti na meza, uchakavu wa miundombinu ya baadhi ya madarasa na kutokamilika kwa uzio na kwamba utatuzi wa changamoto hizo kutaboresha mazingira ya ufundishaji na kujifunza.

“Hapa tumepata meza na viti 100, tunamshukuru mbunge wetu, kwani hii imepunguza upungufu uliokuwepo na sasa upungufu uliyobaki ni meza na viti 100, lakini pia tunaomba uzio wa shule umaliziwe ili kupunguza tatizo la utoro wa wanafunzi”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live