Wanafunzi wa shule ya sekondari Boko Mtambani iliyoko Kinondoni jijini Dar es Salaam, wako hatarini kupata matatizo ya kisaikolojia kutokana na kukosekana kwa uzio kati ya madarasa ya shule hiyo na makaburi yaliyokaribu sana na madarasa hayo.
Akizungumza na EATV Mwalimu mkuu msaidizi wa Shule hiyo Mwalimu Agustina Mhagama, anaeleza kuwa wakati mwingine wamekuwa wakilazimika kuahirisha vipindi ili kupisha shughuli za maziko kuendelea.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyobZainabu Rajab, anaeleza kuwa watoto hao wamekuwa wakiathirika sana kwa kushuhudia vitu vya ajabu, ikiwa pamoja na matambiko na ibada za kumbukumbu za marehemu ambazo zinawaathiri kisaikolojia.