Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shujaa aliyeokoa mwili wa mtoto akataa malipo

Mazishi Binti Moro Shujaa aliyeokoa mwili wa mtoto akataa malipo

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shujaa aliyezama Mto Morogoro wenye kina kirefu cha Maji na kumuopoa mtoto wa darasa la tatu, Sabrina aliyekuwa tayari amefariki dunia baada ya kusombwa na maji.

Juma Sadick maarufu kama 'Juma Vigogo' amefunguka mazito ugumu aliopata kiasi cha kupata mwili wa Mtoto Sabrina.

Kwa ushujaa huo juzi familya ya hayati Sabrina walimuita na kumkabidhi pesa kama shukrani, hata hivyo Juma Vigogo alizikataa pesa hizo akidai yeye alifanya kwa mapenzi na si kwa malipo.

Baada ya kulazimishwa sana Juma alipokea pesa hiyo na kwenda kuzitoa sadaka Msikitini.

”Nyinyi mmefiwa ilitakiwa mimi niwape nyinyi pole kwa kuondokewa na mtoto wenu, kwa kuwa mmenilazimisha sana nahisi nisipopokea hizi pesa nitazidi kuwapa simanzi, hivyo pesa hizi nazichukua napeleka Msikitini,” alisema Juma Vigogo ambaye ni Maarufuni Mkoani Morogoro kwa kukata Miti na kufukua Vigogo.

Sabrina Abdallah alikuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mwere ‘B’, alifariki dunia juzi Dersemba 6, baada ya kuteleza kwenye kina kirefu cha maji ya Mto Morogoro majira ya saa 9 alasiri muda mfupi baada ya kutoka shuleni.

Siku ya tukio, Sabrina baada ya kutoka shuleni na kumaliza kula alkwenda kucheza mtoni na dada yake aitwaye Prinsess mgeni ambapo walikuta maji yamejaa lakini ghafla aliteleza na kusombwa na maji.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walifika mapema eneo la tukio lakini hawakufanikiwa kuuona mwili wa Sabrina ndipo Juma Vigogo alisema kutokana na kasi ya maji, huenda mtoto huyo akawa amesombwa kwenda mbali zaidi.

Juma aliwaacha Maafande wa Faya wakiendelea kumtafuta hapo Top Ten yeye kambia kuelekea bondeni alipofika Daraja la Kichangani kuna watu wanaosha Pikipiki na Magari pembezoni ya daraja hilo, wakamueleza muda huu tumeona mguu wa mtoto ukielea juu ya maji.

Taarifa hizo zilimtia moyo kakimbia hadi daraja la Mafisa Mzambarauni barabara kuu ya Moro-Dar baada ya kama dakika 5 kamuona Sabrina anapita kazama kwenye maji kamuopoa.

Baada ya kumuopoa Kakodi Boda boda kampakata na kuja naye hapa akamkabidhi kwa Maafande wa Faya, wakati anazama kwenye Maji viatu vya Juma Kigogo vilisombwa na Maji kaja hapa akiwa Pekupeku,” alisema Mwenyekiti huyo.

Ifahamike kutoka eneo aliliozama Mtoto huyo nyuma ya baa ya Top Ten mpaka daraja la Mzambarani ni takribani umbali wa Mita elfu Mbili kwa maana ya Viwanja 20 vya Mpira wa Miguu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live