Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shinyanga imepokea tani 100 za mbegu za Mahindi

Mbegu Za Mahindi (600 X 349) Shinyanga yapokea tani 100 za mbegu

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: IPPmedia

Mkoa wa Shinyanga umepokea tani 100 za mbegu za mahindi na Alzeti kutoka kwa wakala wa mbegu za kilimo Agricultural Seed Agency ASA kwa ajili ya kuziuza kwa wakuliwa wa kanda ya ziwa.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema, akipokea mbegu hizo mwishoni mwa wiki, alisema zimekuja katika muda muafaka wa maandalizi ya msimu wa kilimo, na kuwataka wakulima wazitumie ili kufanya kilimo chenye tija na kupata mavuno mengi.

Alisema, maeneo mengi ya Mkoa wa Shinyanga yanakabiliwa na ukame na kwamba mbegu hizo ni mkombozi kwa mkulima, ambazo zikipandwa zinachukua muda mfupi kukomaa na kubainisha kwamba alizeti inachukua miezi minne na mahindi miezi mitatu.

"Tunashukuru kupata mbegu hizi bora kabisa za kilimo na naagiza sasa maofisa ugani muwatembelee wakulima huko maeneo ya vijijini na kuwapatia elimu ya kutumia mbegu hizi pamoja na kulima kisasa ili wapate mavuno mengi na kisha kuondokana na umaskini na baa la njaa hapo baadaye," alisema Mjema.

"Haiwezekani tumeletewa mbegu bora za kilimo, halafu mkoa wetu wa Shinyanga uje kutokea baa la njaa, hili sitakubali nataka tulime kimkakati ili tuwe na chakula cha kutosha," aliongeza.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Mbegu za Kilimo, Dk. Sophia Kashenge, alisema Mkoa wa Shinyanga wameuteua kuwa kituo kikuu cha kusambaza mbegu hizo za kilimo kwa Kanda ya Ziwa.

Alisema kwa upande wa mbegu za alizeti wameleta kilo 20,000, mahindi kilo 89,000, ambazo zinafikia tani 100.

Alisema katika mbegu za alizeti mkulima atauziwa kilo moja kwa Sh. 3,500, mahindi Sh. 2,700.

Chanzo: IPPmedia