Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shilingi bilioni 2.5 zatumika kuboresha barabara mwanza

D066e18df24bf126c66b036d1da994b1.jpeg Shilingi bilioni 2.5 zatumika kuboresha barabara mwanza

Sat, 12 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

ZAIDI ya Sh bil 2.5 zimetumiwa na Wakala ya Barabara Vijijini na Mjini (TARURA) Jijini Mwanza kujenga na kukarabati sehemu miundombinu katika maeneo tofauti hivyo kuwezesha ubora wa huduma ya usafiri.

Akizungumza na HabariLEO jana Jijini Mwanza, Mhandisi wa TARURA Jijini, Danstan Kishaka alisema katika mwaka wa 2020/21 Jumla ya Sh 2,585,003,742.74 zimetumiwa kujenga na kukarabati miundombinu ya barabra katika maeneo tofauti jijini Mwanza.

Kishaka alisema kuwa kazi zilizofanyika na zinazoendelea kutendeka ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, mawe,changarawe, ujenzi wa mitaro na makalvati, kuzibua mifereji na kuziba viraka vya lami.

Alizitaja kata zilizonufaika na huduma hizo kuwa ni Isamilo, Pamba, Igogo, Butimba, Mkolani, Nyamagana, Mabatini,Kishiri, Lwanhima, Mhandu, Luchelele, Buhongwa,Nyegezi, Mkuyuni na Mahina.

Alisema kazi hizo mpaka sasa zimefikia kiwango cha asilimia 95 kukamilika katika ubora unaotakiwa na TARURA ili ziweze kudumu na hivyo kuliepusha taifa na hasara ya ujenzi wa mara kwa mara.

“Wakati tukiwa karibu kumalizika kwa mwaka 2020/21 ninayo imani kazi zetu hizi zitakuwa zimemalizika hivyo nitowe rai kwa watumiaji wa barabara kuutunza Ili zidumu kwa mda mrefu Ili fedha zinazoekekezwa na serikali katika eneo hilo zitumike katika maeneo mengine”.

Aliyataja makampuni yanayofanya kazi hizo kuwa ni Nyanza Road Works, Good Choice S.M Cleaners, Rock Zone Link, AM & Partners, Rasu, Asa General Supplies and Construction na Soro Engineering Works.

Chanzo: www.habarileo.co.tz