Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shilingi bilioni 107 kutekeleza miradi mikubwa Iringa

MSIGWA IRINGA Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema mkoa wa Iringa umepokea jumla ya shilingi bilioni 101.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2021/2022

Amesema hadi kufika mwezi Oktoba 2021 tayari mkoa huo umepokea shilingi bilioni 22.6 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.

"Ipo miradi miradi mikubwa katika mkoa huu ambayo imepangwa kutekelezwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 na tayari umeshapokea shilingi bilioni 22.6 kati ya bilioni 101.7 hii ni miradi mikubwa sio midogo" Amesema Msigwa.

Ametaja miradi hiy kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za lami, ujenzi wa Hospitali Kilolo, Ukarabati wa mradi wa maji wa Isimani-Kilolo, Ujenzi wa Hospitali ya Iringa, Ujenzi wa jengo la Utawala la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Ujenzi wa Chuo cha Veta Pawaga na kumalizia ujenzi wa daraja la Tosamaganga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live