Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shida ya maji UDSM kuwa historia

76687 Udsm+pic

Sun, 22 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Shida ya maji katika Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) itakuwa historia ifikapo Desemba 2019.

Hayo yameelezwa leo Jumamosi Septemba 21, 2019 na Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako wakati akikagua miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa katika chuo hicho.

Amesema mfumo uliopo sasa una uwezo wa kuhifadhi maji lita 45,000 tofauti na mradi wa sasa utakaokuwa na uwezo wa kuhifadhi lita 100,000.

"Kutokana na ukubwa wa chuo hiki uwezo tulionao ni mdogo kwani maji yakikatika unakuwa usumbufu kwa wanafunzi.”

"Lengo la mradi ni kusambaza maji ili kubaki na akiba, utakapokamilika tutakuwa na uwezo wa kutumia zaidi ya siku nne ikiwa yatakatika,” amesema Profesa Ndalichako.

Amebainisha kuwa mradi huo unaogharimu Sh1.8 bilioni  za makusanyo ya ndani ya chuo hicho.

Pia Soma

Advertisement
Msimamizi wa mradi huo, Hellen Twigela amesema mradi huo umefikia asilimia 65 na utakamilika ka ifikapo Disemba mwaka huu uwe umekamilika.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz