Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheikh awataka watanzania kujifunza kwa yanayotokea Libya, Syria

Sat, 16 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.  Sheikh wa Msikiti wa Nunge Dodoma mjini Ahmed Zuber Ahmed amewataka waislam kote nchini kutafakari  kuhusu amani na kuangalia yanayotokea katika nchi yza Libya,Yemen na Syria.

Sheikh Zuber ameyasema hayo leo Juni 15 wakati akitoa salamu za Eid al-Fitr i katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

Amesema kuwa wananchi wa mataifa hayo walitamani kusherehekea sikukuu Eid el-fitr kama wanavyofanya watanzania lakini katika nchi zao amani imetoweka.

“Leo tumefikia mwisho wa safari yetu ya mwezi mmoja wa kufunga ila tutambue kuwa bila amani na umoja hatuwezi kuendelea, lazima tuondoleane mipaka miongoni mwetu ili tuzidi kudumisha amani iliyopo.”

“Tunatakiwa kutambua kuwa damu ikimwagika haifutwi kwa damu bali inafutwa kwa maji, hivyo tuhakikishe kuwa tunadumisha anami huku tukitafakari yanayotokea kwenye nchi za wenzetu,” amesemaSheikh Zuber.

Sheikh Zuber amewataka wazazi na walezi nchini kutambua kuwa serikali ya viwanda haiwezi kuwanufaisha watanzania kama vijana wa kitanzania a hawana elimu.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz