Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sheikh Ponda akamatwa, maandamano Dar

Sheikh Pondaaaa Pondaaaaa.png Sheikh Ponda akamatwa, maandamano Dar

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezima maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja hadi Manzese, huku likikamata baadhi ya viongozi wanaodaiwa kuyandaa akiwemo Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Taarifa za maandamano hayo inayoandikwa kuwa imetolewa na Shura ya Maimamu Tanzania, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii leo Novemba 10, zikieleza kuwa ni maandamano ya kutetea Mamlaka ya Palestina ambayo yalipangwa kufanyika leo saa 7:30 mchana kuanzia Mnazimmoja hadi Manzese.

Kufuatia taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Jumanne Muliro alitoa taarifa kupitia video kwenye mitandao ya jamii akipiga marufuku maandamano hayo.

Baada ya Shekh Ponda kufika, Polisi ambao hawakuvaa sare walimzuia kuongea na waandishi wa habari na kumuamuru kuingia kwenye gari ndogo, huku watu wengine wakitakiwa kupanda kwenye gari ya Polisi.

Viuta vya sasa kati ya Israel na Palestina vilizuka mnamo Oktoba 7, 2023 kufuatia mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas kuanza kushambulia maeneo ya Israel kupitia Gaza na kusababisha vifo kwa raia wa Israel na ndipo Israel kujibu mapigo.

Mpaka sasa takribani Wapalestina 10,800 wameuawa katika vita hivyo wakiwemo watoto zaidi ya 4,200, wanawake zaidi ya 2,700 na wazee zaidi ya 600, huku Waisrael waliouawa wakiwa zaidi ya 1,400.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live