Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shangwe larindima mapokezi ya mhudumu wa afya Kijiji cha Lusalala

Shangwee 3 640x360 Shangwe larindima mapokezi ya mhudumu wa afya Ileje

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya wananchi wa Kijiji Cha Lusalala kata ya Sange wilaya ya Ileje mkoa wa Songwe kujenga zahanati kwa nguvu zao zaidi ya shilingi milioni hamsini waishukuru serikali kuwapelekea mhudumu wa afya.

Wananchi hao wameeleza hayo mbele ya mkuu wa wilaya hiyo Farida Mgomi katika mkutano wa hadhara Novemba 10, 2023 ambapo kilio cha wananchi kukosa mhudumu wa afya licha ya kukamilisha ujenzi wa zahanati yao Kwa 80% pamoja na ujenzi wa nyumba ya mganga.

Akisoma taarifa ya Kijiji hicho kaimu mtendaji wa Kijiji hicho Faraja Mapunda amesema ujenzi wa zahanati ulianza mwaka 2019 baada ya wanawake kuchoka kubebwa kwenye machela pindi wanapotakiwa kwenda kujifungulia zahanati ya Sange na Ngulilo umbali wa zaidi ya Km 5 hivyo kama wananchi wanaiomba serikali iwapelekee mhudumu wa afya.

Kutokana ombi la wananchi hao mkuu wa wilaya hiyo Mhe.Farida Mgomi amewapongeza wananchi hao kwa ushirikiano mzuri na wajumbe wa halmashauri ya Kijiji hicho kujitolea nguvu kazi ya ujenzi huo, hivyo aliwaondoa hofu ya kuwapelekea mhudumu wa afya kwani serikali inatambua na kujali nguvu kazi ya wananchi.

"Niwaondoe hofu wananchi hapa leo nimekuja na mganga mkuu wa wilaya Joyce Ongati atatueleza amejipanga vipi kuhakikisha ombi lenu linapatiwa ufumbuzi kutokana na viongozi wenu kuwasilisha ombi lenu," amesema Mgomi.

Mkutano huo umegeuka furaha Kwa wananchi wa Kijiji hicho  baada ya mganga mkuu  wa wilaya ya Ileje Joyce Ongati kujibu ombi la wananchi hao kwa kumtambulisha mganga mfawidhi wa zahanati Samsoni Lupimo.

Baada ya kutambulishwa mganga mfawidhi zahanati ya Lusalala Samsoni Lupimo amesema hii ni ajira yake ya kwanza atafanya kazi popote bila kujali mazingira ikiwepo zahanati ya Lusalala na kuwaomba wananchi kushirikiana katika kipindi chote cha utumishi kwenye zahanati hiyo.

Baadhi ya wanawake wameonyesha hisia zao huku wakisema Sasa ndo mwisho wao kujifungulia njiani sambamba na kuacha kubebwa kwenye machela na bodaboda ambapo umbali mrefu wa kufuata huduma ya uzazi kufuata zahanati ya Sange na Ngulugulu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live