Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shamba la bangi lateketezwa Mara

Untitled 1 5 Shamba la bangi lateketezwa Mara

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shamba la bangi  hekari mbili limeteketezwa kwa moto katika kijiji cha Tatwe kata ya Goribe wilayani Rorya mkoani Mara katika oparesheni maalum ya tokomeza uhalifu  ikiwa ni pamoja na kuwasaka wezi wa mifugo.

Akizungumza wakati wa kuchoma shamba hilo mkuu wa Wilaya ya Rorya Juma Chikoka amesema  oparesheni hiyo maalumu inalengo la kutokomeza kilimo hicho cha bangi pamoja na uhalifu ambao upo hasa uhalifu wa Mifugo ndani ya wilaya hiyo

Nao viongozi wa serikali ya kijiji cha tatwe wanatoa wito kwa wananchi wao kuacha kujishuhulisha na kilimo hicho cha madawa ya kulevya na badala yake wafanye kilimo cha halali ambacho kitawaingizia kipato.

Aidha mkuu wa Wilaya amesema wanaendelea.kuwasaka watu wanaojihusisha na kilimo hicho cha bangi pamoja na kuendelea kutokomeza wezi wa mifugo ambao wamekuwa wakiwasumbua wananchi kwa kuwaibia mifugo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live