Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shahidi akiri kuidhinisha miamala ya mkurugenzi

Md Pima Shahidi akiri kuidhinisha miamala ya mkurugenzi

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shahidi wa tano katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, DK John Pima na wenzake wawili amekiri kuidhinisha miamala miwili mikubwa ya mteja wake Innocent Maduhu ambaye ni mtuhumiwa namba tatu.

Gerald Lymo (33), Meneja wa Bank ya NMB tawi la Makole Dodoma ameiambia mahakama kuwa aliidhinisha kutolewa kiasi cha Sh milioni 75 kutoka akaunti binafsi baada ya taratibu za kibenki kukamilika.

Vilevile aliidhinidha kiasi cha Sh milioni 17 kutoka kwa mtuhumiwa namba tatu kwenda kwa Anna Kulaya.

Katika kesi hiyo, mbali na Dk Pima watuhumiwa wengine ni Mwekahazina wa jiji hilo Mariam Mshana na mkuu wa idara ya uchumi innocent Muduhu ambao wanakabiliwa na makosa tisa likiwemo kosa la ufujaji na utakatishaji fedha kiasi cha Sh milioni 103.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live