Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh661 milioni zatengwa kuwalipa wananchi kijiji cha Rubwera

Wed, 12 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikaki ya Tanzania itatumia Sh661.9 milioni kuwalipa fidia wananchi wa kijiji cha Rubwera jimbo la Kyerwa mkoani Kagera ili kuondoka katika eneo walilokuwa wakiishi lililochukuliwa na Jeshi la Magereza.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Juni 11, 2019 bungeni jijini Dodoma na naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni akibainisha kuwa Serikali itawalipa wananchi hao wakati wowote kulingana na upatikanaji wa fedha.

Masauni alikuwa akijibu swali la msingi la mbunge wa Kyerwa (CCM),  Innocent Bilakwate aliyetaka kujua lini wananchi wa Rubwera katika kitongoji cha Rwekorongo watalipwa fidia yao baada ya eneo lao kuchukuliwa mwaka 2017.

Hata hivyo,  mbunge huyo alikata majibu hayo kwa maelezo kuwa hayana tija kwa wananchi kwa kuwa suala hilo ni la muda mrefu kwani wanatakiwa kulipwa ili kujipanga kuendeleza maendeo mengine.

 

Katika ufafanuzi wake Masauni amesema Serikali itaendelea kulipa fidia hizo kwa awamu kutegemea na upatikanaji wa fedha kutoka kwenye bajeti ya serikali.

Pia Soma



Chanzo: mwananchi.co.tz