Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh5.2 bilioni kutatua adha ya maji Tabora

Kero Majipic Sh5.2 bilioni kutatua adha ya maji Tabora

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian amesema wilaya za Sikonge na Kaliua zinaongoza kwa kuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji katika mkoa huo.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya utoaji saini mikataba kumi ya miradi ya maji vijijini kwa mwaka wa fedha 2021/22, Dk Batilda amesema Sikonge ndio ina asilimia ndogo kwa upande wa mjini kwa kuwa na asilimia 39 wakati kwa vijijini Kaliua ikiwa na asilimia na asilimia 30.

Amesema kuwa kutokana na miradi hiyo ya maji itakayotekelezwa pamoja na mradi wa maji wa Ziwa Victoria utakaopeleka zitatatua changamoto hiyo.

Amesema kuwa kwa wastani hali ya upatikanaji wa maji kwa mkoa wa Tabora ni asilimia 62.4 kwa upande wa vijijini na mjini asilimia 75.

"Miradi ya maji inayotekekezwa kwa sasa na itakayokuja itafanya hali ya upatikanaji wa maji kuwa nzuri katika mkoa wetu" amesema Dk Batilda

Meneja wa Mamlaka ya maji safi Mijini na vijijini (Ruwasa) mkoa wa Tabora, Mhandisi Hatari Kapufi amesema miradi hiyo ina thamani ya Sh5.2 bilioni na itatekelezwa katika vijiji 44.

"Miradi hii inagosainiwa mara itakapokamilika itaongeza upatikanaji wa maji kwa asilimia nane kwa maeneo ya vijijini" amesema Mhandisi Kapufi

Katibu msaidizi Sekretarieti ya Maadili Kanda ya Magharibi, Gervas Mwaitebele amewataka wakandarasi na viongozi wote kuhakikisha wanakuwa waadilifu katika utekelezaji wa miradi hiyo ya maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live