Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh4.6 bilioni kumaliza tatizo la maji Musoma Vijijini

MAJI 3 Sh4.6 bilioni kumaliza tatizo la maji Musoma Vijijini

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa vijiji vya Mayani, Tegeruka na Kataryo Wilaya ya Musoma mkoani Mara wanatarajiwa kuondokana na adha ya kutumia zaidi ya saa sita kutembea kwenda na kurudi Ziwa Victoria kufuata maji mara utekelezaji wa mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya Sh4.6 bilioni utakapokamilika.

Mradi huo utakaohudumia zaidi ya watu 13,000 unatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Musoma) na unatarajiwa kukamilika Novemba, 2023.

Akitoa taarifa ya utekelezaji leo Oktoba 25, 2023 wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Musoma ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani humo, Mkurugenzi mtendaji wa wa Muwasa, Nicas Mugisha amesema utekelezaji wa mradi huo tayari umefika asilimia 57.1.

New Content Item (1)

‘’Awali kulikuwa na changamoto kadhaa ikiwemo ucheleweshaji wa malipo kwa mkandarasi; lakini kwa sasa fedha zimepatikana na malipo ya zaidi ya Sh1.3 bilioni alizoomba mkandarasi tangu mwezi Juni, 2023 zinatarajiwa kufanyika wakati wowote,’’ amesema Mugisha

Wananchi kicheko

Wakizungumzia katika kijiji cha Mayani kuhusu upatikanaji wa maji kijijini kwao, baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wamesema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji kwa muda mrefu hivyo mradi huo ni mkombozi kwao

Agnes Majura, mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Mayani amesema licha ya kumaliza tatizo la maji umbali mrefu na muda wanaoutumia hivi sasa tutafuta huduma ya maji, kukamilika kwa mradi huo pia utatoa fursa kwa wananchi kujiendeleza kiuchumi kwa kutumia muda mwingi ambao awali waliutumia kusaka maji kushiriki shughuli za uzalishaji mali.

"Saa sita tnazozitumia sasa kufuata maji ziwani tutazitumia kwenye uzalishaji mali; hii itaongeza siyo tu kipato cha watu, bali pia maisha bora kiuchumi na kijamii,’’ amesema Agnes

Kauli hiyo imeungwa mkono na Joshua Manyama huku akiipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi huo aliosema umesubiriwa kwa muda mrefu.

"Hapa kijijini tunakuwa na uhakika wa maji kwenye mabwawa madogo madogo na visima vifupi nyakati za masika; ikifika kiangazi mama na wake zetu hutumia muda mwingi kufuata maji ziwani na hivyo kuathiri shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi. Kukamilika kwa mradi huu ni ukombozi kwa wananchi,’’ amesema Manyama

Amesema muda mwingi wa kufuata maji ziwani siyo tu imeathiri ushiriki wa wanawake katika shughuli za uzalishaji mali, bali pia umesababisha matatizo ya kihusiano kwenye baadhi ndoa kijijini hapo kutokana na baadhi ya wanaume kuwatuhumu wake zao kukosa uaminifu kwenye ndoa kwa kutumia fursa ya kufuata maji ziwani kujihusisha kimapenzi na wanaume wengine.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk Halfan Haule ameutaka uongozi wa Muwasa na mamlaka nyingeine za Serikali kusimamia utekelezaji wa mradi huo kwa wakati na ubora unaolingana na thamani halisi ya fedha za umma zinazotumika kuutekeleza.

Amesema Serikali imetanua idadi ya wanufaika kwa kuhakikisha mradi huo uwanufaisha wananchi katika vijiji jirani zaidi ya sita ambavyo pia vinakabiliwa na tatizo la huduma ya majisafi na salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live