Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh3.1 bilioni zaleta matumaini upatikanaji maji Momba

Vijini Maji.jpeg Sh3.1 bilioni zaleta matumaini upatikanaji maji Momba

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya Sh3.1 bilioni zilizopelekwa wilayani Momba Mkoa wa Songwe zimeanza kuleta matumaini ya upatikanaji wa maji katika maeneo yenye ukame wa muda mrefu.

Mradi huo utaelekezwa katika Kata za Nkangamo na Kakozi ambako Serikali imeanza kutekeleza miradi miwili ukiwamo wa kuchimba bwawa la kuvuna maji ya mvua na kuyahifadhi, kisha kuyasambaza kwa wananchi katika kijiji cha Chiwanda.

Akizungumzia mradi wa ujenzi wa bwawa la kuvuna maji ya mvua, leo Novemba 30, 2023 mbele ya Kamati ya Usalama ya Wilaya Momba, Mhandisi kiongozi Mamlaka ya Rasilimali za Maji Bonde la ziwa Rukwa, Ramadhani Singano amesema mradi huo umeanzishwa kama motisha kwa wakazi wa maeneo yenye ukame wa muda mrefu.

Amesema mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Sh1.3 bilioni, ukikamilika utawanufaisha wakazi wa kijiji cha Chiwanda na vijiji jirani vya Nkangamo na Isanga wapatao 14,449 pamoja na mifugo ipatayo 2,609.

“Maji yatakayovunwa kupitia bwawa hili yatatumika majumbani na kunyweshea mifugo, lakini pia kumwagilia katika mahamba” amesema Singano.

Naye Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilaya ya Momba, Mhandisi Beatus Katabazi, amesema mradi mwingine uko kijiji cha Isanga na unagharimu zaidi ya Sh1.8 bilioni.

Diwani wa Kakozi, Fravian Sichizya amesema wananchi wanapata shida ya maji hasa kipindi cha kiangazi ambako wanachota maji machafu yenye rangi ya udongo, hivyo kukamilika kwa mradi huo utakuwa ukombozi mkubwa kwao.

Mkuu wa Wilaya Momba, Kenani Kihongosi ameagiza watendaji kuongeza kasi katika utendaji ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na wananchi waanze kunufaika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live