Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh160 bilioni zatolewa kujenga vyumba vya madarasa

BASHUNGWA WE Innocent Bashungwa, Waziri wa TAMISEMI

Wed, 28 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tanzania, imetoa Sh160 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 8,000 vitakavyowezesha kupokea wanafunzi 400,000 watakaojiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2023.

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Septemba 28, 2022 na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Amesema kwa mwaka 2023, takribani wanafunzi milioni 1.14 wanatarajiwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza nchini.

“Ikumbukwe wanafunzi hawa ni wale walioanza darasa la kwanza mwaka 2016, mwaka ambao Serikali ilianza utekelezaji wa Sera ya Elimumsingi bila ada Desemba 2015,” amesema.

Amesema idadi hiyo watakaoingia kidato cha kwanza mwakani ni kubwa ukilinganisha na nafasi 454,902 zitakazoachwa wazi na wanafunzi wa kidato cha nne.

Amesema fedha hizo Sh160 bilioni, zimeshainingia kwenye akaunti za shule za sekondari 2,439 zilizoainishwa kuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya kidato cha kwanza 2023.

Amesema fedha hizo zimetumwa na kupokelewa kwenye halmashauri 184 kulingana na upungufu uliowasilishwa na kila halmashauri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live