Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh11 trilioni zatekeleza miradi ya maendeleo Kigoma

Pesa Fedhaddd Sh11 trilioni zatekeleza miradi ya maendeleo Kigoma

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI ya awamu ya sita imepeleka Sh trilioni 11.4 mkoani Kigoma fedha ambazo zimetumika kutekelezaji miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengenye amewasilisha taarifa hiyo leo Januari 23, 2023 kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mohamed Kawaida anayefanya ziara mkoani Kigoma.

Andengenye amesema pamoja na mambo mengine fedha hizo zimetumika kutekeleza miradi ya umeme kiasi cha Sh bilioni 534 ikiwemo umeme wa Gridi ya Taifa kutoka Nyakanazi Sh bilioni 467.3 na uzalishaji wa umeme wa maporomo ya Igamba Sh bilioni 66.7.

Mkuu huyo wa mkoa amesema serikali pia imepeleka mkoani humo kiasi cha Sh trillion 7.32 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa kilometa 506 kutoka Tabora hadi Kigoma na kilometa 242.5 kutoka Uvinza hadi Msongati.

RC Andengenye amesema serikali pia imepeleka mkoani humo kiasi cha Sh bilioni 7.2 za ukarabati wa meli ya MT Sangara, ujenzi wa meli ya abilia/mizigo Sh bilioni 138.6, meli ya mizigo Sh bilioni 146, kiwanda cha meli bilioni 298 na ukarabati wa uwanja wa ndege wa Kigoma Sh bilioni 40.

Sambamba na hilo alisema kuwa serikali pia imewekeza kiasi kikubwa kwenye sekta ya afya ikiwemo kutumia Sh bilioni 36 ujenzi wa tawi la Chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbi (MUHAS), ujenzi, ukarabati na unoreshaji wa miundo mbinu ya afya ya mkoa na kutumia Sh bilioni 5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda.

Akizungumzia suala la miundombinu ya barabara Andengenye alisema kuwa serikali imetoa kiasi cha Sh bilioni 371 kwa Wakala wa Barabara nchini (TARURA) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kiasi cha Sh bilioni 47 huku miradi ya maji ikitumia kiasi cha Sh bilioni 429.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live