Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh11 bilioni kutatua ukosefu wa maji Dar

Dawasapic Data RC Makalla amebainisha kuanza kwa mradi huo

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shilingi bilioni 11 zimetengwa kwa ajili ya kutatua tatizo la maji katika maeneo ya pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, alipofanya ziara katika mradi wa maji wa Kisarawe,unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Dawasa).

Makalla amesema mradi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa hivi karibuni na utakamilika Februari mwakani.

Ametaja maeneo yatakayohusika kuwa ni Temeke, Kigamboni na Ilala, Makalla amewataka wenyeviti wa Serikali ya mtaa kuwahamasisha wananchi kutoa ushirikiano pindi mradi huo utakapoanza.

"Nipongeze kuchukua maji kutoka Ruvu juu, kwani maelekezo ya asilimia nane ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wananchi wanapata maji na kutelekeza kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani inaenda kukamilika," amesema Makalla.

Advertisement

Chanzo: www.tanzaniaweb.live