Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh1,000 kuwapatia chakula wanafunzi mashuleni

Chakula Kanisani Sh1,000 kuwapatia chakula wanafunzi mashuleni

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Kindamba ameeleza umuhimu wa viongozi kusimamia utekelezaji wa maazimio juu ya kuimarisha lishe kwa watoto hasa wenye umri chini ya miaka mitano na kuendelea ili kujenga kizazi kijacho ambacho ni bora.

Kindamba alizitaka halmashauri zote 11 za Mkoa wa Tanga kutekeleza kwa ukamilifu azimio la kuchangia Sh1,000 kwa kila mtoto kwa ajili ya kupata lishe shuleni ili kuimarisha juhudi za kujenga kizazi bora. “Jambo la ukuaji na suala la lishe ni muhimu sana. Tunatengeneza kizazi kizazi kijacho. Lazima tutengeneze kizazi cha watu walio bora kuliko sisi na wao watafanye hivyo hivyo,” amesisitiza.

Kindamba amesema kuwa Watanzania wasiliangalie suala la lishe kwa mtazamo finyu bali kwa mtazamo mpana kwa sababu nchi inataka kujenga kizazi ambacho kinaweza kushindana katika majukwaa ya kimataifa na watoto wa mataifa makubwa. Hivyo, alisema, lazima viongozi na Watanzania kwa ujumla kuhakikisha kuwa wanalipa suala la lishe kipaumbele. “Tusipofanya hvyo tunajitengezea bomu ambalo litatulipukia ikifika wakati kwa kutozingatia maeneo yanayogusa ukuaji wa mtoto,” amesema. Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa hata Rais Samia Suluhu Hassan vipaumbele vyake vyote vimelenga katika suala la kuhakikisha mtoto anakuwa katika mazingira mazuri kwa kutoa fedha katika sekta za maji, afya na elimu. Aliwataka viongozi kushirikiana kuondoa udhaifu katika utekelezaji wa viashiria vilivyowekwa kama vile suala la uundaji wa klabu za lishe shuleni, asilimia ndogo ya viwanda vidogo vinavyoongeza virutubisho katika chakula na asilimia ndogo ya shule zinazotoa lishe shuleni. Aizungumza katika kikao hicho, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Pili Mnyema alisema kuwa pamoja na changamoto zilizojitokeza kiujumla, halmashari nyingi zimefanya vizuri katika utekelezaji wa mipango yakuimarisha lishe ya mtoto. Alisema kuwa hali ya udumavu katika mkoa wa Tanga imepungua kutoka asilimia 34 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 21.4 mwaka 2022 kwa watoto walio katika umri kuanzia sifuri (0) hadi miaka 8 wakati ambapo hali ya uzito pungufu imepungua kutoka asilimia 15.6 hadi kufikia asilimia 11.2 mwaka 2022. “Kama halmashauri zitaendelea kutekeleza afua za lishe kama vile utekelezaji wa azimio la kutenga Sh1,000 kwa kila mtoto hali ya udumavu na ukosefu wa lishe kwa ujumla itaendelea kupungua hususan kwa watoto walio katika umri kuanzi miaka 0 hadi 8,” alisema Mnyema. Mapema, Ofisa Lishe Mkoa wa Tanga, Sakina Mustafa alisema kuwa utendaji wa fedha kwa ajili watoto, utoaji wa chakula shuleni na kutoadhimisha Siku ya Lishe katika vijiji ni changamoto zinazokabili mkoa katika mkakati wa kuboresha lishe ya watoto mkoani Tanga. Aliwataka viongozi wote kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata chakula shuleni ili waweze kusikiliza masomo yao vizuri. Pia alizungumzia hali ya utoaji matone ya Vitamini A kwa watoto walio umri wa mwa 0 hadi miaka 8 alisema kuwa utekelezaji hadi hivi sasa umefikia asilimia 82.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live