Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh trilioni 8 kupeleka Umeme kwenye vitongoji

Ewura Makamba Pic Sh trilioni 8 kupeleka Umeme kwenye vitongoji

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Waziri wa Nishati Januari Makamba amesema serikali inahitaji zaidi ya Sh trilioni 8 kuhakikisha vitongoji vyote nchi nzima vinapata umeme.

Akijibu hoja za wabunge wakati wa mjadala wa mpango wa taifa wa maendeleo kwa mwaka 2021/22, makamba amekili kwamba zoezi la kupeleka umeme katika vijiji kote nchini halijaweza kufikia kila kitongoji.

“Tunakuja na mradi mkubwa. Tunafahamu umeme hautumiwi na kijiji unatumiwa na watu,” amesema na kueleza kuwa Wizara inataka kuainisha mahitaji halisi ili watakaohitaji umeme waweze kubainishwa na kuunganishwa katika ngazi ya kitongoji.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi za serikali, Tanzania ina kadiriwa kuna na vitongoji 64,384 hata hivyo ni vitongo 27,000 tu ndivyo vinapata huduma hiyo ya nishati.

Waziri Makamba amedai kuwa wizara yake pia inakusudia kuwaleta wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme kote nchini kufika Bungeni mwezi Februari ili kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na wabunge.

“Tunatengemea kuwa wakandarasi hao watatumia siku tatu na Mbunge atakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja kubainisha maeneo ambayo bado yanachangamoto,” amesema Waziri Makamba.

Chanzo: www.habarileo.co.tz