Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh milioni 500 kujenga madarasa Nachingwea

F1312ab00f99c35b8e419d7529939edc Sh milioni 500 kujenga madarasa Nachingwea

Wed, 7 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

HALMASHAURI ya Wilaya ya Nachingwea imepanga kutumia mgawo wa mauzo ya mapato ya korosho ya Sh milioni, 500 kwa ujenzi wa madarasa, hosteli na kuboresha majengo yaliyopo yanayohitaji ukarabati.

Aidha, halmashauri hiyo imetenga zaidi ya Sh milioni 200 kutoka kwenye asilimia kumi ya mapato yake ya ndani kwa kipindi cha mwaka 2021 kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali vya wanawake, vijana na walemavu.

Akizungmza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Hassan Rugwa, alisema kuwa kiwango hicho cha fedha kinatokana na makubaliano baina ya halmashauri na wakulima kuhusu kuchangia fedha kuboresha huduma za jamii kutokana na mauzo ya korosho.

Rugwa alisema kiasi hicho cha fedha kimepatikana kutokana na makusanyo baada ya wakulima hao kuuza mazao yao.

Alisema tayari ujenzi wa madarasa hayo umeanza sanjari na kazi ya ukarabati wa baadhi ya majengo yaliyochakaa.

Kuhusu sekta ya afya, mkurugenzi huyo alisema ipo changamoto ya uchache watumishi na wameiomba serikali kuu kusaidia.

Alisema kwa mwaka wa fedha wa 2021, halmashauri hiyo imepanga kukusanya Sh bilioni 2.2 kutokana na vyanzo vyake mbalimbali vya mapato.

Chanzo: www.habarileo.co.tz