Wakala Wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Ruvuma kwa mara ya kwanza wamefanikiwa kurejesha mawasiliano kwa wakazi wa wilaya ya Nyasa na wilaya ya Ludewa mkoani wa Njombe baada ya kukamilisha ujenzi wa daraja la Mto Ruhuhu.
Daraja hilo linakwenda kutatua changamoto za wananchi kwani tangu Tanzania ipate uhuru walikuwa wanatumia ngalawa kuvuka mto huo ambao unawanyama wakali.
Meneja wa Tanroads mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephata Mlavi amesema daraja hilo litakuwa na uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa tani 30 za mizigo na litadumu kwa miaka 100.
Aidha ameongeza kusema kuwa linakwenda kuchochea ukuaji wa uchumi ukizingatia kuna uzalishaji mazao mbalimbali na usafirishaji wa makaa ya mawe.