Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh 7 bilioni kujenga daraja Morogoro

Daraja Daraja (600 X 291) Sh 7 bilioni kujenga daraja Morogoro

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura), imepanga kutumia zaidi ya Sh7 bilioni katika ujenzi wa daraja jipya la Berega wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro.

Ujenzi wa daraja hilo ukioanza baada ya lililokuwepo kusombwa na maji unahusisha ujenzi wa daraja lenye urefu wa meta 140, barabara mkaribio za daraja mete 600 na maboresho ya barabara kutoka Berega kwenda Dumbalume kilometa saba katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.

Hayo yameelezwa jana Jumatano, Februari 22, 2023 wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi iliyofanywa na Bodi ya Ushauri ya Tarura ikiongozwa na mwenyekiti wake, Mhandisi Florian Kabaka.

Mhandisi Kabaka alisema ujenzi wa daraja hilo utaleta manufaa makubwa kwa wananchi wa Berega na maeneo mengine waliokuwa wakipata taabu baada ya daraja la awali kuvunjika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live