Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yazuia matumizi ya msitu Nkamba Katavi

Msituuuu Serikali yazuia matumizi ya msitu Nkamba Katavi

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: Mwananchi

Timu ya Mawaziri wanane wa kisekta iliyotembelea maeneo yenye mwingiliano na mipaka ya hifadhi, imeamuru wakazi wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kutofanya shughuli za kibinadamu katika msitu wa Nkamba ili kulinda mazingira.

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu amesema hayo leo Septemba 28, 2023 kwenye mkutano wa hadhara wakati akitoa mrejesho wa ziara ya mawaziri hao waliofika kujiridhisha maeneo yenye muingiliano na mipaka ya hifadhi katika kijiji cha Kaseganyama na Kasekese.

Amesema uamuzi wa Baraza la Mawaziri kuhusu maeneo ya uhifadhi yameridhia kuwa msitu wa Nkamba katika mipaka yake yote kama ilivyo tangazo la Serikali (GN) utaendelea kuhifadhiwa.

“Hautatumika kwa shughuli za kilimo na zingine za kibinadamu, sehemu ya visima viwili ni sehemu ya msitu wa Nkamba kwa hiyo zisifanyike shughuli zozote za kibinadamu,” amesema Buswelu.

Aidha amewahimiza wananchi wa vijiji vya Kasekese na Kaseganyama kutii uamuzi huo waliousubiri kwa muda mrefu na atakayekiuka atachukuliwa hatua za kisheria.

“Eneo la Visima viwili liliamiwa na baadhi ya watu wamejenga makazi na wengine wanalima, Mawaziri wameamuru lisitumike lipo ndani ya hiadhi ya msitu wa Nkamba,” amesema.

Awali, wakazi wa vijiji cha Kaseganyama na Kasekese miongoni mwa wale waliotakiwa kusubiri tathmini ifanyike upya wakapaza sauti zao wakiiomba Serikali iwaruhusu kulima eneo la visima viwili.

Joseph Benedictor mkazi Kaseganyama amesema ameshangaa kuona mabango yanapelekwa eneo la visima viwili akauliza hao ni watalaam wanakwenda kuangalia mipaka?

“Wanafuatana na Mwenyekiti kwenda kuweka mabango bila kutupa majibu, tunakuomba Mkuu wa Wilaya utatue mgogoro huu wa ardhi sisi tunasubiri watalaam wapitie mipaka,” amesema Benedictor.

John Madoshi mkazi Kasekese amesema “mnatusumbua sana sasa hivi mmekuja kuweka bikoni mmeanza kusogeza tena huku zamani ilikuwa mbele mnachotaka ni nini tutakula wapi jamani?” amehoji.

Oktoba 12 mwaka jana timu ya mawaziri hao ilitembelea vijiji hivyo kujiridhisha mipaka yake ikawaahidi wakazi hao kupata mrejesho baada ya tathmini upya kufanyika.

Chanzo: Mwananchi