Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yawasikiliza wananchi wa Tandale

Wananchi Tandale Gst Serikali yawasikiliza wananchi wa Tandale

Sat, 20 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye serikali imesikia kilio cha wananchi na kuweka matuta katika barabara ya kiboko baa iliyopo Tandale Muhalitani ambapo wananchi wa mtaa huo waliifunga barabara hiyo kwa siku tatu wakishinikiza kuwekwa matuta kutokana na kutokea kwa ajali za mara kwa mara

Wakizungumza nasi wananchi hao wamekishukuru kituo hiki kwa kuripoti habari hiyo na serikali kuona na kwenda kuweka matuta manne ambayo sasa wamesema yamesaidia kupunguza mwendo wa vyombo vya usafiri vinavyotumia barabara hiyo

Hata hivyo mmoja wa viongozi wa wananchi hao amesema #EATV imefanya jitihada kubwa ambazo zimesaidia serikali kufahamu changamoto iliyopo katika mtaa huo kwani ajali hizo zilizokuwa zinatokea zimekuwa zikihatarisha usalama wa maisha ya wananchi

Hata hivyo mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Tandale Muhalitani amewataka madereva wa vyombo vya moto wananitumia barabara hiyo kuacha kuendesha vyombo hivyo kwa mazoea kwani madereva wengi hasa wa bodaboda wamekuwa wakianguka kutokana na kutotanbua kama barabara hiyo tayari imeshawekwa matuta

Baada ya jitihada za kumtafuta meneja wa wakala wa barabara mijini na vijijini wilaya ya Kinondoni ili kuzungumzia suala hilo la uwekaji matuta lakini jitihada hizo zimegonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live