Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaupatia mkoa Ruvuma mabilioni

D3bfefab7b5a5a1fb40ecf89e6f3c4ab Serikali yaupatia mkoa Ruvuma mabilioni

Wed, 16 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA mweza wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano serikali imeupatia Mkoa wa Ruvuma Sh bilioni 163 kutekeleza shughuli za maendeleo.

Samia alisema hayo jana katika Viwanja vya Mnada wa Zamani wakati akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Madaba wilayani Songea katika mkutano wa kampeni kuomba kura za urais, wabunge na madiwani.

Alisema fedha hizi zimesaidia kuboresha maisha ya wananchi na kuharakisha maendeleo ikiwemo sekta za maji, barabara na afya. Kati ya fedha hizo, Sh bilioni 1.7 zimepelekwa Halmashauri ya Wilaya Madaba kukarabati vyumba vya madarasa na mabweni na ujenzi wa maabara katika shule za sekondari.

Alisema serikali pia imeendelea kuboresha huduma za kijamii ikiwemo miundombinu ya barabara, maji na afya.

Aidha, alisema serikali itaendelea kuboresha mtandao wa barabara na sasa imeshamaliza upembuzi yakinifu kwa ajili ya kujenga upya barabara ya Songea hadi Makambako yenye urefu wa kilometa 296.

Samia alisema katika sekta ya afya, serikali imeupa mkoa huo Sh bilioni 17.6, ambazo Halmashauri ya Madaba imepokea Sh milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo kipya cha Afya Mtyangimbole, Sh milioni 400 Kituo cha Afya Madaba na imetenga Sh bilioni tatu kujenga hospitali ya wilaya.

Chanzo: habarileo.co.tz